TANZANIA YA KESHO
Saturday, April 27, 2013
Waandamana kuhusu Korosho Tanzania, Takriban nyumba 20 zimeteketezwa katika maandaman
Takriban nyumba 20 zimeteketezwa katika maandamano yaliyofanywa na wakulima wa Korosho pamoja na waandamanaji wengine Kusini mwa Tanzania.
Hii ni kwa mujibu wa mbunge mmoja wa eneo hilo
Mbunge huyo, Faith Mitambo alisema kuwa majengo mawili nyumbani kwake mjini Liwale, yalichomwa na kuwa nyumba zingine mali ya baadhi ya wanachama wa chama tawala CCM ziliteketezwa.
Uharibifu huo ulianza baada ya wakulima kulipwa kiasi kidogo cha pesa ikilinganishwa na zile walizokuwa wamekubaliana kulipwa na serikali baada ya kuiuzia mazao yao mwaka jana.
Polisi zaidi wamepelekwa katika eneo hilo kuzuia ghasia zaidi.
Bi Mitambo, aliyekuwa mjini, Dodoma, wakati huo aliambia BBC kuwa alikuwa anazuru eneo bunge lake kudadisi hali ilivyo.
Alipokea habari kuwa waandamanaji waliokuwa wanajumuisha vijana , walianza kufanya fujo vijijini mnamo Jumanne asubuhi hadi walipofika mjini Liwale saa za jioni.
Mkaazi mmoja wa mji huo aliambia BBC kuwa mnamo Jumatano kulikuwa na hali ya wasiwasi mjini humo na kwamba polisi walikuwa wamewarushia gesi ya kutoa machozi wandamanaji ili kuwatawanya.
Maelfu ya wakulima wadogo wadogo wanaopanda Korosho nchini Tanzania na ambao huvuna mazao yao mwezi Oktoba, huyauza kwa mashirika mbali mbali kwa bei waliyokubaliana.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam, Erick Nampesya anasema kuwa wakulima walikubaliana kulipwa shilingi 1,200 pesa za Tanzania kwa kila kilo ya korosho hizo.
Mwishoni mwa mwaka jana, wakulima walilipwa sehemu ya deni lao.
Lakini pale waakilishi kutoka kwa mashirika walipokwenda katika wilaya ya Liwale, kuwalipa sehemu ya mwisho ya deni lao, wakawa wamebadilisha makubaliano waliyokuwa wameafikiana.
Wakulima walilipwa nusu au chini ya nusu ya deni lililokuwa limesalia, baada ya kuambiwa kuwa bei ya Korosho ilikuwa imeshuka sana katika soko la kimataifa.
Wanasiasa wakuu ambao wakulima hao wanawalaumu kwa kukosa kuwasaidia ndio walikuwa wamewaelekezea ghadbabu zao
Wakulima wamekuwa wakilalamika kuhusu msukosuko wa bei za Korosho ambayo huathiriwa zaidi kulingana na msimu.
Thursday, February 7, 2013
WANAUME WATAKIWA KUACHA TAMAA ZA FISI. NANI KASEMA BOFYA HAPA
Wito huo ulitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummi Mwalimu wakati akijibu swali
la Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Mary Mwanjelwa (CCM) ambaye alihoji kama
Serikali haioni kuwa ni wakati mwafaka kubadilisha Sheria ya Ndoa ili
umri wa kuolewa utoke miaka 14 na kuwa 18.
Katika swali hilo Mwanjelwa aliitupia lawama
Serikali kuwa imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa vifo vya wanawake
ambao vingi vinatokana na kuzaa katika umri mdogo.
Naibu Waziri alisema kifungu cha 13 (1) cha Sheria
ya Ndoa sura ya 29, kinasema kuwa mwanamume mwenye umri wa chini ya
miaka 18 na mwanamke mwenye umri wa chini ya miaka 15 hawaruhusiwi
kufunga ndoa na mtu yeyote lakini akasema kifungu cha 13 (2) kinaipa
Mahakama mamlaka ya kufungisha ndoa baada ya maombi maalumu.
Alisema Mahakama inaweza kutoa kibali hicho endapo
waombaji wamefikisha umri wa miaka 14 na Mahakama ikiridhika kwamba
yapo mazingira maalumu yanayohitajika wenye umri huo kufunga ndoa.
“Vilevile kifungu cha 17 (1) kinampa fursa mtoto
wa kike mwenye umri wa chini ya miaka 18, kupata ridhaa ya kuolewa
kutoka kwa mzazi wake au mlezi wake endapo baba au mama watakuwa
wamefariki,” alisema Mwalimu.
Hata hivyo alikiri kuwa Serikali inatambua kuwa
watoto wengi wamekuwa wakiolewa chini ya umri uliowekwa na sheria na
mara zote hatua za kisheria zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya wazazi,
walezi na wanaume wanaowaoa wasichana hao.
Arusha; Njaa yasababisha wanaume kutelekeza familia
WAKATI njaa ikizidi kuathiri maeneo mbalimbali nchini, baadhi ya
wanaume katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wamekimbia familia
zao kutafuta chakula.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa baadhi ya
wanaume wameshindwa kuhudumia familia zao na kulazimika kwenda nchini
Kenya na baadhi ya mikoa nchini kusaka vibarua.
Mwandishi wa gazeti hili alifanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa eneo hili wakiwamo wanawake ambao wanaelezea hali ilivyo.
Mwandishi wa gazeti hili alifanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa eneo hili wakiwamo wanawake ambao wanaelezea hali ilivyo.
Jirani na Bibi Lembirika nakutana na msichana
mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 19 anajitambulisha kuwa ni Narik
Saruni, mgogoni ana mtoto mdogo, Grace Noah.
Nalazimika kumuuliza baba yake na mtoto yupo wapi,
anajibu kwa Kiswahili cha taabu kuwa amekwenda kutafuta kazi ya ulinzi
nchini Kenya.
Narik mkononi, ana mfuko na ninapomuuza ana nini, anajibu kuwa ana mboga za porini anauza kila fungu moja Sh100. Anajieleza kuwa akipata pesa hizo, ananunua mahindi na kusaga ili kupata uji wa kunywa yeye na mtoto wake.

“Kila siku nakwenda porini kuchuma mboga na
nikipata naleta huku madukani kuuza kwa siku naweza kupata Sh800 ambayo
naitumia kununua kopo moja la mahindi,”anasema.
Familia zaishi kutegemea mchicha pori
Nakwenda katika Kijiji cha Irkepus,Kata ya Nainokanoka, hapa nakutana na kundi la watoto, wakiwa na bibi zao na mboga za majani mkononi, nasimama na kuwaliza, lakini hawajui Lugha ya Kiswahili.
Nakwenda katika Kijiji cha Irkepus,Kata ya Nainokanoka, hapa nakutana na kundi la watoto, wakiwa na bibi zao na mboga za majani mkononi, nasimama na kuwaliza, lakini hawajui Lugha ya Kiswahili.
Hapa nampata Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji
cha Irkepus, Thomas Ole Njoro anamwita mmoja wa wanawake hao ambaye
anajitambulisha kwa Kimasai kuwa ni Topoi Lembaya ila hajui miaka
aliyozaliwa. Hata hivyo, kwa kumtazama ni bibi kizee mwenye umri kati ya
miaka 75 hadi 85, kwani hata kutembea kwake anatumia fimbo. Kupitia
mwenyekiti huyo wa kitongoji nawauliza, walichobeba ni nini, bibi huyo
anajibu kwa Kimasai kuwa ni mchicha wa porini ambao wanachuma kwa ajili
ya chakula.
Anasema hayo ndio maisha yao kwa takriban mwezi
sasa kwani, mahindi ya msaada ambayo yalitolewa na Serikali hivi
karibuni pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wamemaliza, hivyo
hawana chakula tena.
Bibi huyo anasema anaishi na wajukuu hao, kwani baba yao, Lesika Lemoro ameenda nchini Kenya kutafuta kazi.
Familia nyingi ambazo ninazitembelea ninakutana na
wanawake na watoto huku wanaume wakielezwa kuwa wameondoka kwenda Kenya
na Arusha na mikoa mingine kutafuta kazi. Mpaka wa Kenya upo jirani na
vijiji hivi.
Anasema maisha yao ni taabu, kwani hawana ng’ombe
na sasa wamegeuka ombaomba katika maboma ya jirani. Mwenyekiti huyo wa
Kitongoji, anakiri familia hiyo, kukabiliwa na njaa kwani anasema
Desemba 20, mwaka jana ndiyo ilikuwa mara yao ya mwisho kupata chakula
cha njaa.
Anasema katika kitongoji chake, kaya 379
zinakabiliwa na upungufu wa chakula, lakini ni kaya 125 tu ndizo
zilipatiwa chakula kiasi cha kilo tisa za mahindi kwa kila kaya.
Mahindi ya kuchemsha yaokoa familia
Natembea kwenye maboma ya Kimasai katika kijiji hicho, naingia kwenye moja ya maboma haya napiga hodi hakuna ambaye anaitika, lakini naingia ndani nakutana na moshi mkali.
Hapa nabaini kuwa kuna watu, lakini kutokana na nyumba za jamii hii za kimasai kuwa za asili, zenye vidirisha vidogo sana, nashindwa kuvumilia na kutoka nje na ndipo bibi kizee anatoka ndani.

Nashindwa kuzungumza naye na hapa pia nalazimika
kumwita Mwenyekiti wa kitongoji ili aje kuwa mkalimani, anafika na
kumuuliza bibi anafanya nini ndani. Bibi huyu mwenye umri kati ya miaka
80 hadi 90 akiwa haoni, anajitambulisha kuwa ni Saleita Nanga, anasema
anapika chakula cha wajukuu wake wanne.
Hapa napata shauku ya kuomba nikione chakula
hicho, Mwenyekiti wa kitongoji analazimika kuingia ndani ya boma hili na
anatoka na sufuria yenye mahindi yanayocheshwa.
Hapa nabaini ni mahindi ambayo hayajachanganywa na kitu yametoka kwenye magunia na moja kwa moja kuingizwa katika maji machache na kuchemshwa.
Hapa nabaini ni mahindi ambayo hayajachanganywa na kitu yametoka kwenye magunia na moja kwa moja kuingizwa katika maji machache na kuchemshwa.
Nanga anasema hicho ndio chakula cha siku hiyo na
muda huo ni saa 11:30 jioni anasema wajukuu zake, tangu wanywe chai
asubuhi hawajaonja kitu kwani hana uwezo wa kupata chakula zaidi ya mara
mbili.
Chakula cha msaada chashindwa kusambazwa
Katika kijiji hiki pia nakutana na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kipenjiro,Saiboko Kimirei ambaye eneo lake ndio linatajwa kukabiliwa kuna wananchi wengi wanaokabiliwa na njaa kali.
Kimerei anasema hali ya usambazaji wa chakula katika eneo lake ni gumu kwani maeneo mengi barabara hazipitiki kabisa.

“Kwangu hali ni mbaya sana, ukifika unalazika
kutembea kwa miguu hadi kilomita 20 kuonana na wananchi kwani hakuna
barabara ya gari,” anasema Kimerei.
Anasema tayari ametoa taarifa ngazi za serikali
juu ya hali hiyo na ugumu wa kusambaza chakula, lakini bado hajapewa
majibu ya uhakika.
Ofisi ya Waziri Mkuu yawaokoa Enduleni
Siku ya pili mapema asubuhi, nakwenda katika Kata ya Enduleni kata hii ndio anatoka Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Saning’o Ole Telele.
Siku ya pili mapema asubuhi, nakwenda katika Kata ya Enduleni kata hii ndio anatoka Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Saning’o Ole Telele.
Hapa napokelewa na sura za matumaini za wanawake,
vijana, watoto na wazee, kwani siku hiyo, walikuwa wanapokea chakula cha
msaada kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, kiasi cha tani 70 za mahindi.
Mwenyekiti wa kijiji hiki, Julius Peter anasema,
wamepokea tani 70 za mahindi ambayo wanauza Sh50 kwa kilo moja. Hapa ni
heka heka ya kugawana mahindi tu na wakati zoezi likiendelea naona
makundi ya watoto wenye makopo wakizoa chini, mahindi kidogo
yanayomwagika.
Hawa ni watoto wa jamii ya kimasai na wanazoa
mahindi huku, wakigombania na hivyo nabaini pia katika eneo hili hali ya
uhaba wa chakula ipo.
Nalazimika kuhojiana na makundi mbalimbali ya
wanawake na vijana na hapa, nampata Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wa
CCM wa Kata hiyo ya Enduleni, Emilisiana Munga.
Munga anasema, kata hiyo yenye watu zaidi ya 12,000 nusu yao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Munga anasema, kata hiyo yenye watu zaidi ya 12,000 nusu yao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Thursday, March 1, 2012
vip ukichaguliwa kuwa mmoja wa tume ya kuunda katiba utafanyaje kw manufaa ya Tanzania ya kesho?
Naamu watanzania wenzangu habari za mishuhuriko ya hapa na pale katika kujipatia chochote kitu na ujenzi wa taifa kwa ujumla,
Leo nataka kujua kama watanzania na vijana wa taifa la sasa na kesho, iwapo utapata fursa ya kuteuliwa kwenye tume ya Rais katika kukusanya maoni kwa ajili ya katiba mpya utawasaidiaje wa tanzania kuwasilisha maoni yao? au utatumia nafasi hiyo kujipatika kipato kwa ajili ya njaa ya leo nakusahau watanzania wenzako wa kesho?

Sunday, January 8, 2012
mwendo wa kinyonga na maendeleo ya tanzania
mwaka 2011 tumeshuhudia majigambo ya viongozi wa nchi yetu ya tanzania wakisema tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele. lakin nikiwa kam mtanzania naweza kuwa na mtazamo tofauti na kaulimbiu hiyo ya serikari kwa mambo yafuatayo
miaka hamsini ya uhuru yenye miundo mbinu mibovu, naam nikiwa mkoani tabora nimejikuta katika hali ya maisha hatarishi hasa katika suala la barabra ipitayo manyoni Itigi kiukweli kama unaelekea Samunge yaani barabar ni yavumbi mpaka kerooo na isitoshe kunakipande kama cha km 10 ama kilitumika kuombea kula za ubunge ama ngazi ya juu kwani ni bonge la danganya toto,
mfumoko wa bei za vyakula ni balaaa, hali inayo mfanya babu na bibi yangu wa igowole waweze kuishi katika (Abject Poverty) umaskin ulio kithili kiasi cha kula mlo mmoja ama kutokula kabisha. swali je ni tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele kimaendeleo ama kiamskini

Subscribe to:
Posts (Atom)