Wito huo ulitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummi Mwalimu wakati akijibu swali
la Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Mary Mwanjelwa (CCM) ambaye alihoji kama
Serikali haioni kuwa ni wakati mwafaka kubadilisha Sheria ya Ndoa ili
umri wa kuolewa utoke miaka 14 na kuwa 18.
Katika swali hilo Mwanjelwa aliitupia lawama
Serikali kuwa imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa vifo vya wanawake
ambao vingi vinatokana na kuzaa katika umri mdogo.
Naibu Waziri alisema kifungu cha 13 (1) cha Sheria
ya Ndoa sura ya 29, kinasema kuwa mwanamume mwenye umri wa chini ya
miaka 18 na mwanamke mwenye umri wa chini ya miaka 15 hawaruhusiwi
kufunga ndoa na mtu yeyote lakini akasema kifungu cha 13 (2) kinaipa
Mahakama mamlaka ya kufungisha ndoa baada ya maombi maalumu.
Alisema Mahakama inaweza kutoa kibali hicho endapo
waombaji wamefikisha umri wa miaka 14 na Mahakama ikiridhika kwamba
yapo mazingira maalumu yanayohitajika wenye umri huo kufunga ndoa.
“Vilevile kifungu cha 17 (1) kinampa fursa mtoto
wa kike mwenye umri wa chini ya miaka 18, kupata ridhaa ya kuolewa
kutoka kwa mzazi wake au mlezi wake endapo baba au mama watakuwa
wamefariki,” alisema Mwalimu.
Hata hivyo alikiri kuwa Serikali inatambua kuwa
watoto wengi wamekuwa wakiolewa chini ya umri uliowekwa na sheria na
mara zote hatua za kisheria zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya wazazi,
walezi na wanaume wanaowaoa wasichana hao.
No comments:
Post a Comment