music

HANS%20MBEDULE%20BLOG

Sunday, January 8, 2012

mwendo wa kinyonga na maendeleo ya tanzania

mwaka 2011 tumeshuhudia majigambo ya viongozi wa nchi yetu ya tanzania wakisema tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele. lakin nikiwa kam mtanzania naweza kuwa na mtazamo tofauti na kaulimbiu hiyo ya serikari kwa mambo yafuatayo
miaka hamsini ya uhuru yenye miundo mbinu mibovu, naam nikiwa mkoani tabora nimejikuta katika hali ya maisha hatarishi hasa katika suala la barabra ipitayo manyoni Itigi kiukweli kama unaelekea Samunge yaani barabar ni yavumbi mpaka kerooo na isitoshe kunakipande kama cha km 10 ama kilitumika kuombea kula za ubunge ama ngazi ya juu kwani ni bonge la danganya toto,
mfumoko wa bei za vyakula ni balaaa, hali inayo mfanya babu na bibi yangu wa igowole waweze kuishi katika (Abject Poverty) umaskin ulio kithili kiasi cha kula mlo mmoja ama kutokula kabisha. swali je ni  tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele kimaendeleo ama kiamskini

Monday, January 2, 2012

katiba ijayo na maendeleo ya nchi yetu

kwa kuanzia napenda kuwapongezeni kwa kuchaguliwa tena kuingia katika huu mwaka mteule 2012
 mwenyezi mungu awajaalie maisha marefu yenye kujiletea maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.
 nirudi kwenye lengo la maada ya kuu, ikiwa mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba tarajiwa iwejee, kunajambo nataka tushee pamoja, kiukweli tanzania itaweza kuendelea iwapo itapatikana katiba yenye makusudi na wananchi wake na sio katiba yenye kuwapa maendeleo ya wachache na wenye feza kwa na kuwaacha wanyonge wakiendelea kudidimia kimaisha, ombi kwa wananchi wenzangu tusijifiche bali tutoke na kujitokeza kwa wingi kuchangia japo kwanafasi finyu tuliopata kwa uzio wa kutojadili mambo mengine ambayo tume ya kukusanya maoni haita yawasilisha hatakama yatajadiliwa. habibu ya rejea kama mswada uliopitishwa ulivyo